BAADA ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye, mshindi wa milioni 10 amepatikana kupitia droo ya Shinda Mahela na Championi ambaye ni Kizito George Chuka.

Droo hiyo iliyochezeshwa mbele ya Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao kwenye Viwanja vya Mbagala- Zakhem jana Jumanne.

Akizungumza Kizito ambaye ni makazi wa Kawe jijini Dar alipopigiwa simu na muendeshaji wa shughuli hiyo MC Chaku, mshindi huyo alikuwa ndani ya daladala hivyo hakuwa na mengi ya kuongeza zaidi ya kushukuru kwa kujinyakulia kitita hicho.

Kizito, 43 alionekana kufurahia kutokana na sauti yake kusikika akichekelea na haijafahamika kama aliwasilimulia abiria wenzake aliokuwa nao ndani ya daladala hiyo.

Hata hivyo keshokutwa Alhamisi anatakiwa kuja Ofisi za Global Publishers kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuchukua mkwanja wake huo.

“Nimefurahi sana lakini sasa hivi nipo ndani ya daladala naomba muda nikifika nitakupigia,” alisema Kizito.
Washindi wengine ambao walipatikana siku hiyo ni Athuman Yusuph, 40, mkazi wa Mwanza aliyejinyakulia shuka za kisasa na Amiri Kinguaba, 60 aliondoka na simu kali aina ya Samsung Galaxy.
MC Chaku (kushoto) akiwa na mmoja ya wakazi wa Mbagala tayari kwa kuchagua mshindi wa Championi Shinda Mahela.
Msimamizi wa Bodi ya Bahati Nasibu, Mrisho Milao (kushoto), Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (katikati) na kulia ni Ofisa Masoko wa Shinyanga Emporium, Herman Bernard wakiendelea kufuatilia droo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...