Taasisi ya RAFIKIELIMU FOUNDATION kupitia mradi wa ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI NA VIJIJINI, inatangaza nafasi za MAFUNZO
YA UALIMU WA UJASIRIAMALI .
Wahitimu wa mafunzo haya watapata nafasi ya kufanya kazi kwa kujitolea kama waalimu wa ujasiriamali katika MRADI WA ELIMU YA UJASIRIAMALI MIJINI & VIJIJINI.
IDADI YA NAFASI :
Nafasi 5 katika kila kata ya jiji la Dar Es salaam.
SIFA ZA MWOMBAJI :
1. Awe raia wa Tanzania mwenye elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
2. Awe mkaazi wa Dar Es salaam.
3. Awe na wito wa kufanya kazi ya ufundishaji.
4. Awe tayari kufanya kazi kwa kujitolea kama mwalimu wa ujasiriamali katika kata yoyote ya jiji la Dar Es salaam.
MAFUNZO yatatolewa kwa mwezi mmoja kuanzia tarehe 02 MACHI 2014 katika Chuo Chetu kilichopo katika eneo la CHANGANYIKENI.
ADA YA MAFUNZO : MAFUNZO HAYA YANATOLEWA BURE.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...