Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Ndugu Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM mjini Dodoma leo Februari 16,2014.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Ndugu Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa NEC mara baada ya kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ambapo alisema Kamati ya Maadili imeuliza masuala mazito na maswali magumu yanayohusiana na uvunjaji wa maadili ya uongozi wa chama chetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Watanzania wenzangu wale wenye upendo na malengo mazuri ya nchi yetu hii aliyotuachia Baba wa Taifa JK Nyerere.

    " HIVI IKULU KUNA BIASHARA GANI PALE NZURI YA KUPAKIMBILIA HADI MTU AFIKIE HATUA YA KUTOA VIJIPESA ILI AWEZE KUINGIA IKULU?" Hii ni nukuu ya Baba wa TAIFA letu na muasisi wa chama chetu kipenzi cha CCM " ZIDUMU FIKRA ZAKE SAHIHI MWANZILISHI"

    Baba wa Taifa kuna kipindi alitoa hutuba na kutuasa kuwakwepa kama ukoma wale viongozi ambao wako tayari kutoa mapesa ili waingia kule IKULU. Mwalimu aliwashangaa sana na kutuasa sisi WENYE NCHI kuwakwepa wale walafi wa madaraka.
    Juzi Mh sana MEMBE aliitwa na ile kamati maalumu ya MAADAILI ya CCM chini ya Mh sana MANGULA kujieleza juu ya uvunjifu wao wanaoufanya wa kuanza kampaign kabla ya muda wake. Hivi kweli kiongozi mwenye niya ya kweli anaweza kufanya kile kilichofanywa na wale wote ambao wameanza campaign zao kabla ya wakati? huu si utovu wa nidhamu na uvunjaji wa kanuni za taratibu zilizowekwa za chama?, HIVI leo wanapuuza hili je wakiingia pale ikulu wanapopapigania na hata kwa kumwaga mijipesa si watatukanyaga vichwani na kutupuuza siye tuliyowakweka pale?
    Mimi siyo mwanasiasa na wala sikusudii kuingia kwenye duru za kisiasa bali niMTANZANIA MSOMI na mwenye upendo wa dhati na nchi yetu. Chama chetu lazima kiwe makini haswa kama kinataka kuingia tena IKULU 2015, Hawa waliovunja utaratibu ni lazima waadhibiwe kwa mujibu wa kanuni zilizopo na mojawapo ni kuwaengua katika kinyang'anyiro cha urais ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizi.
    Pia ni vyema kuhoji wale wanaotumia MAPESA KWA HARAMBEE waitwe na waulizwe kwa nini wanatoa mijipesa hiyo na source yake ni wapi? je wanatumia hizo pesa watazirudishaje? wasijetuuza sisi wenye nchi kwa hao wanaowapa mapesa hayo.

    Ni muhimu kuheshimu kanuni zilizopo na moja ya sifa ya kiongozi safi ni yule anayeheshimu KANUNI na MIONGOZO iliyowekwa. Pendekezo langu ni kuwaengua kabisaa hawa jamaa na tutafute wale walio safi hawana kashfa na hawavunji kanuni. Nadhani chama chetu kina watu wengi na competent kufanya yale mazuri haina haja ya kuwataja majina ila wanajulikana watu SAFI.

    Baba wa Taifa alituasa tuwaogope kama ukoma watu wanaotumia pesa na kupigania kwenda IKULU na kama CCM inataka kumuenzi BABA WA TAIFA na kujisafisha mbele yetu sisi wenye nchi basi wafanye maamuzi magumu sasa na mojawapo ni kuwaengua hawa jamaa.
    Kama tulishindwa kusimamia "KUJIVUA GAMBA" basi hili tusishindwe ili tupate RADHI ZA WAASISI WETU.

    KIDUMU CHAMA CHETU MAKINI NA ZIDUMU FIKRA ZAKE SAHIHI MZEE WETU JK NYERERE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...