KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka na Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions imewaomba wadau wenye nia ya kufanikisha maendeleo ya matamasha hayo kuwasaidia katika muendelezo wa matamasha yanayoandaliwa na kampuni hiyo, Aprili  mwaka huu kampuni hiyo iko mbioni kuandaa Tamasha la Pasaka.  

Kutokana na hali hiyo, wadau mbalimbali ambao wamepata kutoa ahadi za namba mbalimbali katika matamasha hayo wameombwa kutekeleza ahadi zao ili zitumike katika malengo yaliyokusudiwa. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema wadau mbalimbali wa muziki wa Injili, wakiwemo baadhi ya viongozi wamekuwa wakitoa ahadi ambazo utekelezaji wake umekuwa mgumu.
“Wapo baadhi ya watu wanakuja katika matamasha yetu, wanatoa ahadi nzito hasa za fedha, lakini tamasha likishamalizika wanashindwa kutekeleza ahadi zao na ndiyo huwaoni tena, tunashukuru wapo wengine huwa wepesi kutimiza walichoahidi.“Huwa haya matamasha tunayaandaa kwa malengo maalum, ukitaja ahadi yako huwa tunaipa thamani kubwa na ukishindwa kuitimiza unatuangusha na hilo ndilo linatuharibia sana mipango yetu,” alisema Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi.

Aliwaomba baadhi ya viongozi na wadau wengine ambao wamepata kutoa ahadi mbalimbali kwenye Tamasha la Pasaka kuhakikisha wanatekeleza ahadi zao kama walivyozitoa na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya kuwataja majina kwani wenyewe wanajitambua.
“Tunaamini pengine wana mambo mengine ndiyo sababu tumeandika barua kuwakumbusha wakati huu tukielekea katika maandalizi ya Tamasha la Pasaka,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani mie siku zote huyu ndani huwa mnaleta habari za MSAMA kuwa ni promota. Sasa hapa anapoomba udhani tena inakuwaje? Au yeye sio promota?

    ReplyDelete
  2. Sema wewe nami pia nimeshangaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...