Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,Emmanuel Switta akimpeleka markiti Golikipa wa timu ya Simba, Yaw Berko kwa mkwaju mkali wa Penati na kuiandikia timu yake bao la pili katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa mchezo Simba wamelala kwa Bao 3 - 2.Picha na Othman Michuzi.

Wachezaji wa timu ya JKT Ruvu wakishangilia mara baada ya kuitandika Simba bao la pili.
 Golikipa wa Timu ya Simba,Yaw Berko akiruka bila mafanikio ya kudaka shuti kali lililopigwa na Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,Emmanuel Switta na kuingia kimiani moja kwa moja na kuiandikia timu yake bao la tatu dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imefungwa bao 3 - 2.
 Nahodha wa timu ya JKT Ruvu,Amos Mgisa akiangalia namna ya kumtoka beki wa Simba,William Lucian wakati wa mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara,uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.katika mchezo huo Timu ya Simba ililala kwa Bao 3 - 2.
 Beki wa Timu ya Simba,Donald Mosoti (kulia) akichuana vikali na mshambuliani wa timu ya JKT Ruvu,Iddi Mbaga.
 Salum Machaku wa JKT Ruvu (kulia) akionyesha uwezo wake mbele ya Beki wa Simba.
Kufungwa kubaya jamaniiiii...... Pichani ni Beki wa Timu ya Simba William Lucian  akiwa amekaa chini mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.
Madaktari wa timu ya JKT Ruvu wakitoka uwanjani kutoa huduma ya kwanza. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Tunataka ushindani wa namna hii, siyo Timu kongwe kuwa zinashinda au kutoa sare kibao mpaka ligi inakosa ushindani.

    Mdau
    Ligi ya Premium England

    ReplyDelete
  2. Alaah....kumbe Ankal ni wa mitaa ya Jangwani, sikuwaga najua vile, naona dalili za ushabiki katika kichwa cha somo hapo juu.....naona pia kuna chembe chembe za unazi hapa.....Lakini siyo vibaya.....kitu kama unakipenda kwanini ufiche hisia zako?

    ReplyDelete
  3. I think Simba have some serious mental issues to sort out!

    ReplyDelete
  4. Ahhh, Simba marijoooo!

    Simba mnafungwa hadi na Maafande?

    ReplyDelete
  5. Simba S.C Kwishney!!!

    ReplyDelete
  6. Ohooo Majeshi yana nguvu si mchezo!

    Hivi Simba mnafikiri ule uhuni wenu wa Msimbazi mtaweza mbele ya Askari?

    ReplyDelete
  7. sijui nitoke timu?

    ReplyDelete
  8. Mshambuliaji wa Ruvu aliyekuwa amevaa jezi #29 aangaliiwe anaweza kusaidia safu ya Ushambuliaji ya Taifa Stars.Ni mrefu,ana mbio na mipira ya juu anaiweza,anatumia akili.

    SIMBA:Pamoja na kufungwa,kuna mgomo baridi au?Ukiondoa wachezaji wa kulipwa tu,wachezaji wazawa hawakuwa kwenye "mood" ya mchezo utadhani walilazimishwa kucheza.Hii ni tathmin yangu binafsi,nilikuwemo Uwanjani

    David V

    ReplyDelete
  9. Wachezaji wanasema hawamtaki kocha na wana madai mengi kwa uongozi kiasi kwamba hawaamini uongozi tena wanaona wanadangaywa na msimu unakwisha, ukizingatia kawaida ya timu zetu hizi mbili msimu ukiisha wachezaji hawakumbukwi tena haswa wale watakaoachwa, kwa hiyo Simba wasitegemee ushindi kwa hali hii!!

    ReplyDelete
  10. Hapa ndio pale UKOMO WA HIRIZI UNAPO GONGA MWAMBA!

    Mfuateni Babu mkadai fedha zenu arudishe.

    Babu amewadanganya Wana Msimbazi.

    ReplyDelete
  11. Wana Msimbazi ni bora muwepe mpira kwapani muanze Umachinga Mtaani kwenu.


    Mpira umesha washinda!

    Mnafungwa hadi na Askari?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...