Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,Emmanuel Switta akimpeleka markiti Golikipa wa timu ya Simba, Yaw Berko kwa mkwaju mkali wa Penati na kuiandikia timu yake bao la pili katika Mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara,uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa mchezo Simba wamelala kwa Bao 3 - 2.Picha na Othman Michuzi.

Wachezaji wa timu ya JKT Ruvu wakishangilia mara baada ya kuitandika Simba bao la pili.
Golikipa wa Timu ya Simba,Yaw Berko akiruka bila mafanikio ya kudaka shuti kali lililopigwa na Mchezaji wa Timu ya JKT Ruvu,Emmanuel Switta na kuingia kimiani moja kwa moja na kuiandikia timu yake bao la tatu dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara,uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imefungwa bao 3 - 2.
Nahodha wa timu ya JKT Ruvu,Amos Mgisa akiangalia namna ya kumtoka beki wa Simba,William Lucian wakati wa mchezo wao wa ligi kuu Tanzania Bara,uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.katika mchezo huo Timu ya Simba ililala kwa Bao 3 - 2.
Beki wa Timu ya Simba,Donald Mosoti (kulia) akichuana vikali na mshambuliani wa timu ya JKT Ruvu,Iddi Mbaga.
Salum Machaku wa JKT Ruvu (kulia) akionyesha uwezo wake mbele ya Beki wa Simba.
Kufungwa kubaya jamaniiiii...... Pichani ni Beki wa Timu ya Simba William Lucian akiwa amekaa chini mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya JKT Ruvu.

Madaktari wa timu ya JKT Ruvu wakitoka uwanjani kutoa huduma ya kwanza.
Tunataka ushindani wa namna hii, siyo Timu kongwe kuwa zinashinda au kutoa sare kibao mpaka ligi inakosa ushindani.
ReplyDeleteMdau
Ligi ya Premium England
Alaah....kumbe Ankal ni wa mitaa ya Jangwani, sikuwaga najua vile, naona dalili za ushabiki katika kichwa cha somo hapo juu.....naona pia kuna chembe chembe za unazi hapa.....Lakini siyo vibaya.....kitu kama unakipenda kwanini ufiche hisia zako?
ReplyDeleteI think Simba have some serious mental issues to sort out!
ReplyDeleteAhhh, Simba marijoooo!
ReplyDeleteSimba mnafungwa hadi na Maafande?
Simba S.C Kwishney!!!
ReplyDeleteOhooo Majeshi yana nguvu si mchezo!
ReplyDeleteHivi Simba mnafikiri ule uhuni wenu wa Msimbazi mtaweza mbele ya Askari?
sijui nitoke timu?
ReplyDeleteMshambuliaji wa Ruvu aliyekuwa amevaa jezi #29 aangaliiwe anaweza kusaidia safu ya Ushambuliaji ya Taifa Stars.Ni mrefu,ana mbio na mipira ya juu anaiweza,anatumia akili.
ReplyDeleteSIMBA:Pamoja na kufungwa,kuna mgomo baridi au?Ukiondoa wachezaji wa kulipwa tu,wachezaji wazawa hawakuwa kwenye "mood" ya mchezo utadhani walilazimishwa kucheza.Hii ni tathmin yangu binafsi,nilikuwemo Uwanjani
David V
Wachezaji wanasema hawamtaki kocha na wana madai mengi kwa uongozi kiasi kwamba hawaamini uongozi tena wanaona wanadangaywa na msimu unakwisha, ukizingatia kawaida ya timu zetu hizi mbili msimu ukiisha wachezaji hawakumbukwi tena haswa wale watakaoachwa, kwa hiyo Simba wasitegemee ushindi kwa hali hii!!
ReplyDeleteHapa ndio pale UKOMO WA HIRIZI UNAPO GONGA MWAMBA!
ReplyDeleteMfuateni Babu mkadai fedha zenu arudishe.
Babu amewadanganya Wana Msimbazi.
Wana Msimbazi ni bora muwepe mpira kwapani muanze Umachinga Mtaani kwenu.
ReplyDeleteMpira umesha washinda!
Mnafungwa hadi na Askari?