Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Pereira Silima akizindua rasmi Jengo la Kituo cha Polici cha Natta Wilayani Serengeti huku Mkurugenzi Mkuu wa Grumeti Fund,Bw. Brian Harris akishuhudia. Kituo hicho cha Polisi cha kisasa kimegharimu shilingi Milioni 273 ambazo zimetolewa na Grumeti Fund ikiwa ni pamoja na nyumba za kuishi familia mbili za Polisi na mfumo wa kuvuna maji.
Naibu Waziri Mambo ya Ndani,Mh. Pereira Silima akikata utepe kufungua rasmi Kituo cha Polisi cha Natta wilayani Serengeti ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa Grumeti Fund kwa gharama ya shilingi Milioni 272 ikiwa ni pamoja na nyumba ya kuishi Askari kwa familia mbili na mfumo mzima wa uvunaji maji. wengine pichani toka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, SACP Ferdinand Mtui, Mkurugenzi Mkuu wa Grumeti Fund,Bw. Brian Harris,Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,John Henjewele, Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki na Naibu Kamishina wa Polisi,DCP Sospeter Kondela.
Kikundi cha Ngoma za asili cha Natta Wilayani Serengeti kikitumbuiza katika sherehe za makabidhiano na ufunguzi wa Kituo cha Polisi cha Natta wilayani Serengeti Mkoa wa Mara kilichojengwa kwa ufadhili wa Grumeti Fund kwa gharama ya shilingi Milioni 273. 
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Abdulrahman Kaniki (kulia) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Serengeti,Bw. Jumanne Kwiro mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha Polisi cha Natta,Wilayani Serengeti mkoani Mara.
Mkurugenzi Mkuu wa Grumeti Fund,bwana Brian Harris (kushoto) akimwonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia amebobea katika mambo ya Misitu na Uhifadhi,Mh. Pereira Silima ramani ya Ecologia ya Mbuga ya Hifadhi ya Serengeti na Mapito ya Wanyama ya kila mwaka,walipokutana katika loji ya kifahari ya Sabora inayomilikiwa na Singita Grumeti Reserves alipotembelea kikazi mwishoni mwa wiki.
Viongozi Wakuu wa Rrumeti Fund wakijipanga kumsubiri Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Mh. Pereira Silima alipotembelea Wilaya ya Serengeti hivi karibuni. kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu mpya wa Grumeti Fund,Dk. Timothy H. Tear,Msimamizi Mkuu wa Miradi ya Grumeti Fund,Bw. Richard Ndaskoi, Mkurugenzi Mkuu wa Grumeti Fund anayemaliza muda wake,Bw. Brian Harris na Meneja wa Uhifadhi wa Grumeti Fund,Bw. Ami Seki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...