Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43. 
 Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe  wilayani Manyoni  zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida. 
 Mtu mmoja  George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno  hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria. 
 Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata  ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.
"Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.
Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na majangili wilayani humo.
Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo na pembe za Faru jijini London, Uingereza.
Katika mkutano huo amependekeza kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Blog ya jamii,leo nilikuwa sehemu fulani jijini Dar mikiwa 'naamsha popo' nimemuona Rais wetu Kikwete akiwa anahojiwa na mwandishi machachari wa BBC swahili Zuhura? Yusuph jijini London leo.Clip hiyo imerushwa na kituo maarafu sana cha TV Tanzamia chenye makao yake makuu jijini Mwanza.Kuna suala fulani kaliongea Rais wetu sikulielewa vizuri kwa sababu ya hao POPO kichwani mwangu.Itafutwe hiyo clip,tuulize maswali. ni masuala muhimu ya kuhusu huu Ujangili.Again,media zetu 'zimelalal sana.

    David V

    ReplyDelete
  2. Naomba isiwe 'tokomeza ujangili' bali igeuzwe kuwa 'tokomeza majangili' maana hawa ni wauwaji wakubwa.

    Au kwa kuwa viumbe hivi haviwezi kujitetea ndiyo maana hawa wauwaji wanawafanyia hivi?

    Mulaanike kwa Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
  3. Atakayekamatwa na nyara hizi naye auwawe; kwani naye anakuwa ameua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...