Jeshi la polisi mkoani SINGIDA limekamata vipande 21 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43.
Nyara hizo za serikali zimekamatwa katika kijiji cha Mwamagembe wilayani Manyoni zikisafirishwa kwenda Itigi, mkoani Singida.
Mtu mmoja George James amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na meno hayo ya tembo yakiwa yamehifadhiwa katika mabegi mawili ya kusafiria.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kizuizi cha idara ya maliasili kilichoko katika kijiji Ukimbu, kata ya Mgandu, wilayani Manyoni akiwa katika gari aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T797CQL.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida RPC Geofrey Kamwela (katika video) amesema vipande hivyo 21 vina thmani ya zaidi ya shilingi milioni 43 na vyote vimehifadhiwa katika kituo cha polisi wilayani Itigi.
"Meno haya yanaashiria kuuwawa kwa tembo wanne", alisema Kamanda James.
Vitendo vya ujangili wilayani MANYONI vimekuwa vikiongezeka ambapo mwaka 2013 askari mmoja wa jeshi polisi alipoteza maisha katika mapambano na majangili wilayani humo.
Tukio hili la limekuja wakati leo Rais Jakaya Mrisho Kikwete amehudhuria mkutano maalumu wa kupambana na ujangili na biashara ya meno ya tembo na pembe za Faru jijini London, Uingereza.
Katika mkutano huo amependekeza kupigwa marufuku biashara hiyo ili kuweza kudhibiti ujangili duniani kote.
Blog ya jamii,leo nilikuwa sehemu fulani jijini Dar mikiwa 'naamsha popo' nimemuona Rais wetu Kikwete akiwa anahojiwa na mwandishi machachari wa BBC swahili Zuhura? Yusuph jijini London leo.Clip hiyo imerushwa na kituo maarafu sana cha TV Tanzamia chenye makao yake makuu jijini Mwanza.Kuna suala fulani kaliongea Rais wetu sikulielewa vizuri kwa sababu ya hao POPO kichwani mwangu.Itafutwe hiyo clip,tuulize maswali. ni masuala muhimu ya kuhusu huu Ujangili.Again,media zetu 'zimelalal sana.
ReplyDeleteDavid V
Naomba isiwe 'tokomeza ujangili' bali igeuzwe kuwa 'tokomeza majangili' maana hawa ni wauwaji wakubwa.
ReplyDeleteAu kwa kuwa viumbe hivi haviwezi kujitetea ndiyo maana hawa wauwaji wanawafanyia hivi?
Mulaanike kwa Mwenyezi Mungu.
Atakayekamatwa na nyara hizi naye auwawe; kwani naye anakuwa ameua
ReplyDelete