Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi Tigo wamezindua huduma ya kuweka
na kutuma pesa kupitia simu za mkononi. Lengo kubwa la huduma hii ni kuwezesha huduma za kibenki
kuwafikia wateja kwa ukaribu na urahisi zaidi.
Huduma hii mpya inawawezesha wateja wote wa NMB na Tigo kuweka na kuhamisha pesa kutoka
kwenye akaunti zao za Tigo Pesa kwenda kwenye akaunti zao za NMB. Vilevile, mteja anaweza kuweka
na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Tigo Pesa. Huduma hii
inafanyika kwenye simu za mkononi na utoaji wa fedha unafanyika kwa Wakala yeyote wa Tigo Pesa.
Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa kitengo cha Athari wa NMB,
Tom Borghols (kati) na Mkuu wa kitengo cha huduma ya Tigo Pesa, Ruan Swanepoel wa kwanza
(kulia) wakiweka sahihi mkataba wa kutoa huduma za NMB kwa kupitia Tigo Pesa . Huduma ambayo inamwezesha mteja wa NMB mobile kutuma fedha kwenda Tigo Pesa na mteja wa Tigo Pesa kuweka
fedha kwenye akaunti ya NMB. Kushoto akishuhudia ni Mkuu wa kitengo cha Huduma Binafsi wa
benki hiyo, Abdulmajid Nsekela.
Kaimu Afisa Mkuu mtendaji wa NMB ambaye pia ni Afisa Mkuu wa kitengo cha Athari wa NMB, Tom
Borghols (kushoto) na Mkuu wa kitengo cha huduma ya Tigo pesa, Ruan Swanepoel wakibadilishana
mkataba wa ushirikiano utakao muwezesha mteja wa NMB mobile kuweka na kuchukua pesa zake
mahali popote kupitia mawakala wa Tigo Pesa nchini na mteja wa Tigo Pesa kuweka fedha kwenye
akaunti ya NMB.
Makato ni shingapi
ReplyDelete