Jahazi lililokamatwa na madawa ya kulevya.
ZAIDI ya kilo 200 za madawa ya kulevya aina ya Heroin yamekamatwa na kikosi cha polisi wanamaji katika Bahari ya Hindi yakisafirishwa kutokea nchini Irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na Pakistani.
Kamanda wa polisi kikosi cha wanamaji Bw. Mboje Kanga ameeleza kuwa tukio hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku ambapo waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala Kingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya, Bw. Godfrey Nzowa amesema jahazi hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosi cha polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.
Chanzo: ITV
Ohhh huu Uchumi wa Unga makubwa tutayashuhudia!
ReplyDeleteYaani umbali uliopo kati ya Iran na TZ na dhoruba ya Bahari lakini vidume kwa kuiska Dola wamakakamaa na safari ngumu saaana kwnye Jahazi tena bovu hadi wanakaribia kuingia Tanzania?
Hawa Jamaa ni vishoka sana!
ReplyDeleteInabidi Marekani iwape Uraia na wawaingize ktk Jeshi la Polisi wa bahari US-COAST GUARD!, ama kwa uchache wapewe Nyota zao za vyeo mabegani kwa kusafiri safari ngumu namna hiyo tena kwenye jahazi la kawaida kabisa!
Dunia inabidi itazame kwa jicho la 3 kwa biashara hii ya kisasa ya unga.
ReplyDeleteUchumi wa unga unachangiwa na mengi mfano.
1.Mgawanyo usio sawa wa fursa.
Wakazi wa dunia wanaamua kuchukua njia rahisi ingawa ya hatari ili kufikia malego ya kimaisha kwa kuwa jamii imegawanyika kwa wengine kukosa kabisa mgawanyo wa fursa ikiwemo kufanya biashara ya kaiwada hivyo baada ya kukosa nafasi ktk Plan-A(Biashata mafenesi, na mazao) wanahamia Plan-B(unga na Uhalifu).
2.Upendeleo na Madaraja.
Kwa kutokana na sababu ya juu No.1 pia wanaona pana kundi la jamii linahodhi kila kitu na kuwa wanakosa Ushindani Huru (FAIR COMPETITION) ktk shughuli karibu zote za kiuchumi.
3.Kodi na Urasimu ktk biashara za kawaida.
Kodi imekuwa ni kikwazo za ustawi wa kibiashara dunia nzima wakati pana nchi zingine unakuta Kodi inakuwa kubwa zaidi ya Faida ya biashara hivyo ukichanganya na Kudorora kwa Uchumi biashara za kawaida zinakuwa hazilipi na watu kuamua kuingia ktk biashara za gizani kama Unga ambazo hazina kigezo cha Ushindani Huru na hazitozwi Kodi.