Hili ni eneo la Ubungo ambalo limekuwa na wimbi kubwa la wafanya bishara wadogo wadogo kuegesha biashara zao za kila aina pembezoni mwa njia za wapita kwa miguu jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Licha ya usumbufu na kero hiyo, eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi sana, limekuwa ndio maskani kwa vibaka ambao hujipatia kipato chao bila hata ya jasho kwa kujichanganya humo kama raia wa kawaida na kufanya wizi.

Wakizungumza watumiaji mbalimbali wa barabara hiyo wamelilalamikia Jiji na Manispaa husika kwa kushindwa kuwataftia eneo husika wafanyabiashara hao wadogo wadogo na kwamba kutokana na uzembe huo mkubwa wa kutowazuia nao wameamua kuendelea kuleta kero

"Eneo hili kwa kweli linatia Aibu sana kwa sababu hapa ndipo Lango kuu la kuingia jijini na mara watu wanapo ingia wanakutana na kero hii ambayo mimi binafsi naita ni uchafu, nasikitika sana kuona Jiji na Halmashari husika wameshindwa kabisa kudhibiti na kuwataftia eneo husika hii ni aibu" 

Alizungumza mmoja wa watumiaji wa barabara hiyo ambaye hupita mara kwa mara.  
 Hii ndiyo hali Halisi ya eneo kutoka Ubungo Darajani karibia na mitambo ya Gesi hadi eneo la watu wanaopandia magari ya kwenda Mwenge? Je Halmashauri ya Jiji hamlioni hili? Je Manispaa husikia nanyie hamlioni hili? Au hili ni eneo halali limepitishwa kwa ajili ya kufanya biashara hizi?

 Hawa nao wanauza Viatu pande hizi kwa bei nafuu...
 Wengine wanauza samaki katika eneo ambalo kiafya sio sahihi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. wanatafuta hela ya kula na kulipa pango ya chumba; ukiwafukuza wataenda wapi; wawe vibaka/majambazi?Afadhali ya hiyo kuliko kuwa kibaka au jambazi?Tunachoomba hali hiyo iondolewe sambamba na hao watu kuwahakikishia wanapata njia ya kuweza kuishi na familia zao na mahitaji mengine ya binadamu, shule, n.k.

    ReplyDelete
  2. Kutafuta hela ya kula siyo sababu ya kuvunja sheria

    ReplyDelete
  3. MICHUZI NAOMBA USINIBANIE..

    Jambo hili linasikitisha sana. Viongozi wetu siku zote wanafanya ziara nchi za watu lakini hawajifunzi. Lakini siamini tatizo kama hili ni la kwenda kujifunza nje ya nchi. Viongozi lakini siku wanaimba vijana mjiajiri lakini hawatengenezi mazingira mazuri ya kujiajiri. Huu umekuwa kama wimbo. Hawa vijana mmeisha fahamu kuwa wanapenda sehemu zilizo karibu na vituo vya usafiri kama vituo vya mabasi. Sasa kwa nini Serikali isije na mkakati wa kuanza kutenga maeneo maalum karibu na vituo vya mabasi yaliyopimwa na kuandaliwa kwa ajili ya hawa vijana. Maeneo hayo yakitengwa na kuzungushiwa uzio vijana hawa watakwenda humo kwa sababu haitakuwa mbali na msongamano wa watu. Mnapoongelea kutengeneza maeneo mazuri ya uwekezaji ni kwa ajili ya wazungu tu? Tukiendeleza sera hizo daima tukiulizwa pamoja na kukua kwa uchumi kwa nini watu ni maskini jibu litakuwa hata mimi sijui. Tubadilike tukiona tatizo tusitafute simple solution. Tuanze sera hii ya kujenga maeneo ya biashara ndogondogo karibu na vituo vikubwa vya mabasi na tutafanikiwa kuwaondoa moja kwa moja kutoka barabarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...