Hii ni video mpya ya msanii mpya wa Tetemesha Entertainment aitwaye BARAKAH da PRINCE. Wimbo unaitwa JICHUNGE. Video ilifanyika Dar na kuongozwa na director kutoka Arusha, NISHER.
Leo 10.03.14 ndio tunaiachia rasmi, lakini audio itatoka rasmi wiki ijayo Jumatatu 17.03.14.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wimbo mzuri,lakini nyie vijana wa muziki wa kizazi kipya kuna haja ya kukaa chini na kufikiria kitu hiki.Tanzania tuna ngoma za kiasili kibao kutoka kila kona.Kwanini msichukue ngoma nzuri moja ya asili(beats zake)wote mkatengeneza muziki wake kwa ala hizi za kisasa kwa style tofauti tofauti?Na mnacheza kama ngoma ile ya asili inavyochezwa.Afrika ya kusini wanafanya hii.Wakiamua KWAITO,wanamuziki wanapiga mapigo ya kwaito kwa styles tofauti tofauti lakini inabaki kuwa kwaito,bubble gum music,nk.Wenzenu wa Afrika ya magharibi wana mapigo yao mfano Azonto, Skelewu, Alingo.Tunataka mtu akisikia muziki fulani aweze kuutambua kwamba ni wa Tanzania.Tukose vazi la Taifa na tukose Muziki wa Taifa?

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...