Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya NBC wakibeba gunia la unga tayari kwenda kutoa msaada kwa wagonjwa wanawake waliolazwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na kuwajali wanawake wenzao walio katika shida.
Mmoja wa maofisa waandamizi wa Benki ya NBC, Sarah Laizer , akikabidhi jora la khanga kwa Msaidizi wa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Kansa ya Ocean Road, Sr. Genoviva Mlawa (kushoto) pamoja na vitu vingine vilivyotolewa na wanawake hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake hao wakiandaa khanga tayari kwenda kuwakabidhi wagonjuwa wanawake waliolazwa katika hospitali hiyo.
Haikuwa Dar es Salaam pekee kwani hapa wafanyakazi wa Benki ya NBC Mkoani Singida nao walitembelea katika Hospitali ya mkoa huo na kwenda kutoa aina mbalimbali za misaada.
Binafsi nimeanza kutambua uwepo wa siku hii kwa mara ya kwanza 2004 nilipoanza kuishi Ulaya kutokana na jinsi ilivyokua ikipewa nafasi na thamani kwa wenyeji,licha ya nafasi na thamani hiyo mara nyingi zawadi kwa walengwa zilihusisha mtu na mtuwe yaani kumpa ua,kumtoa out na kutakiana salam za heri ngazi ya familia au rafiki wa karibu, hii ina akisi zaidi aina ya maisha ya wenzetu.Nimeguswa na nimependezwa mno jinsi sherehe hizi zilivyofanikishwa nyumbani, nasi pia tumeziendesha kivyetuvyetu kwa kuakisi staili yetu ya kiafrika zaidi(upendo na kujaliana).Nimeona akina dada Shamimu, hawa wa NBC nao..ni vizuri kwa staili kama hii kwa wakati ujao tukawaangalia pia wale wa vijijini kwa kuwafariji,wengi wao wapo ktk hali ngumu.Nawapa hongera wote kwa mazuri mliyoyafanya.
ReplyDelete