Mwananchi juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga, akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza. 
Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake.
Huku baadhi yao wakiwa wamejitosa kufanya uokoji wa mali, wananchi wengine kama kawaida yao walikimbilia  eneo la ajali kushuhudia moto huo uliokuwa ukivuma kuashiria hatari na eneo hilo si salama.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pole zao waliopata mkasa huu.

    Huduma za zimamoto ziwe karibu hata kama ni za makampuni binafsi, kulipana kunaweza kuwa baadaye baada ya tukio lakini huduma iwepo.

    ReplyDelete
  2. Miaka mingi iliyopita nilikuwa nafanya kazi katika hospitali moja ya ndugu zetu wamanga uarabuni. Wakati huo ulikuwa wakati ambapo jamaa walikuwa waanza kuacha kutumia mikaa na kuanza matumizi ya majiko ya gesi.Palikuwa na ajali nyingi sana. Hao wauzao majiko hayo huko Bongo, hala hala wafundisheni ndugu zetu matumizi ya majiko hayo na njia za kupunguza eksdenti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...