Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kesho anatarajiwa kuifungua rasmi barabara ya Mkata - Handeni ambayo ujenzi wake umekamilika kwa kiwango cha lami. 
Kwa muibu wa taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi, Barabara hii ina urefu wa kilometa 53.2. 
 Akiwa Wilayani Handeni, Rais Kikwete ataifungua pia barabara ya Korogwe – Handeni ambayo vile vile imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. 
Barabara hii ina urefu wa kilometa 65. Katika hatua nyingine mnamo tarehe 24 Machi 2014 siku ya Jumatatu, Mhe. Rais ataweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara kati ya Korogwe na Mkumbara yenye urefu wa kilometa 76.
Taswira ya sehemu ya mkeka wa Mkata-Handeni ambao utafunguliwa rasmi na Rais Kikwete kesho


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera serikali yetu kwa kutambua umuhimu wa miundo mbinu.

    ReplyDelete
  2. Kwetu kuzuri jamani. Angalia hicho kijani mpaka raha. Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...