Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akiongea katika mkutano a Mazungumzo ya usuluhishi wa mgogoro wa mpaka baina ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa yameanza leo Jijini Maputo, Msumbiji kwa kuzikutanisha pande zote mbili za mgogoro huo.
Mazungumzo hayo yaliyopo chini ya Jopo la Usuluhishi linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joachim Chissano akisaidiwa na Mhe. Thabo Mbeki Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini na Mhe. Festus Mogae Rais Mstaafu wa Botswana yaliwapa nafasi pande zote mbili kutoa tamko rasmi kabla ya usuluhishi kuanza.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo hayo yanoyotarajia kuchukua siku mbili umeongozwa na Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Anna K. Tibaijuka, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Frederick M. Werema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dr. David S. Mayunga, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na wataalamu wengine kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
Aidha ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo haya umejumuisha Wabunge wawili kutoka Kanda ya Ziwa ambao ni Mhe. Kapt. John Komba na Mhe. Deo Filikunjombe.
Hapa chini ni tamko rasmi la Tanzania Kama lilivyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe.
Well constructed arguments.. I hope we will hear what Malawi will have to say too
ReplyDeleteSipati picha kuwa watu wa mbambabay wakitaka kitoweo au kuogelea ziwani waende Blantyre kuchukua viza!
ReplyDeleteyour excellence minister of foreign affairs....we thank you for your logical presentation
ReplyDelete