Hakika baada ya muda si mrefu ujao jiji la Dar es salaam litakuwa na sura mpya kabisa kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara mpya ya mabasi yaendayo haraka. Hapa ni Magomeni mapipa kwa Mcheni ambako kila upande panajengwa kingo za ukuta mkubwa utaosaidia kuzuia mmomonyoko
Kwa Macheni siku hizi hapapo tena...
Ukuta wa Berlin?
Ama kweli haswaaa huo ni ukuta wa Berlin ndani ya Dar Es Salaam.
ReplyDeletemaana Wajenzi ni Kampuni ya Ujerumani STRABAG-AG sasa wameona watukumbushe Historia!
Hapo na bado ndio kwanza alfajiri kuelekea Uchumi wa Oil and Gas!
ReplyDeleteHii ndio sura mpya ya nchi nzima JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Mara kwa mara na Mungu atusaidie!
Mhe. Raisi Kikwete ameingia Madarakani mwaka 2005.
ReplyDeleteKipindi hicho mwaka 2005 na hapo kabla hatukua na kasi hii ya maendeleo ya 7% kwa mwaka, lakini miaka mitatu baadaye mwaka 2008 Tanzania inagundulika kuwa na kiwango kikubwa cha LNG Gas, idadi kubwa sana ya Dhahabu, Uranium, Steel( Chuma) na madini mengi sana ya thamani !
Hivyo tuache ubahili ni wazi Raisi Jakaya Kikwete ameingia na neema zake!
Hizi barabara zinajengwa miaka mingapi? Mtengenezaji 1 waharibifu milion...big up kikwete
ReplyDeletezinajengwa Kwa kodi zetu, huo uharibifu ni ujinga tu wa asilimia kubwa wa taifa hili, angalau walipa kodi si wananchi wote bali wachache sana katika hili Taifa lenye idadi kubwa ya watu, na hao ndi waharibifu wa mali hizi za umma
ReplyDelete1.Ukuta wa Berlin!? Watu tuliouona tunajua kuwa watu walio upande mwingine wa ukuta walikuwa hawaruhusiwi kwenda upande wa pili. Je hapo DSM watu hawaruhusiwi kupenyeza upande mwingine??
ReplyDelete2.Je huo utajiri tuliobarikiwa wanafaidi Wabongo wote wa
mijini na vijijini??
3.Je watoto wetu wanasoma kwenye madarasa mazuri(hasa vijijini)etc,etc.
Hivyo tusijilegeze,as we are still far to run to.