MBUNGE WA MTERA,LIVINGSTONE LUSINDE NA MBUNGE WA MOSHI MJINI MHE PHILEMON NDESAMBURO AMBAO PIA NI WABUNGE WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA WAKIAGANA MARA BAADA YA KUAHIRISHWA KWA SEMINA YA KUANDAA KANUNI ZITAKAZO TUMIWA WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE MAALUMU LA KATIBA MJINI DODOMA.
.jpg)
MHE.OLE SENDEKA AKICHANGIA MSWADA WA KANUNI ZITAKAZO TUMIKA WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE MAALUMU LA KATIBA JANA JIONI.
MHE.JAMES MAPALALA AKIWELEKEZA JAMBO MJUMBE MWENZAKE KWA KIDOLE WAKATI WA SEMINA YA KUJADILI RASIMU YA KANUNI ZITAKAZO TUMIKA WAKATI WA KIKAO CHA BUNGE MAALUMU LA KATIBA. PICHA NA DEUSDEDIT MOSHI WA GLOBU YA JAMII, KANDA YA KATI
wakati nchi kadhaa za afrika zimejadili na kubadili katiba kiurahisi, Tanzania kama kawaida yetu tunaendelea kupoteza mamilioni kuwalipa machopopo wajumbe hawa na wale wanakamati hawa na wale, haya yataisha lini?
ReplyDeleteNi juzi tu tumesoma hapa kuna shule nzima ina mwalimu mmoja, mamilioni yanayotumika katika kujadili katiba mpya zingelitumika vyema kama zingelielekezwa kwenye elimu, kuongeza mishahara ya walimu, kujenga mashule imara na kufundisha walimu wapya.
Zoezi zima lilaloendela kwa sasa halina umuhimu wowote katika suali la kubadili katiba ila ni njia tu ya wenye matumbo makubwa kuzidi kujilumbikizia posho za kila aina.
Watazanzania tutaamka lini?
Tutaamka baada ya kupata katiba yenye mustakabala mwema zaidi kwa vizazi vijavyo
ReplyDelete