Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na
wanahaabari (hawapo pichani) kuhusu vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamlaka hiyo.Kulia ni Afisa
Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Frank Mvungi.
Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza, akionesha moja ya
vipodozi vilivyopigwa marufuku na mamalaka hiyo kinachotumiwa na wanawake kukuza makalio.
Baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Afisa Uhusiano wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA),
Gaudensia Simwanza (hawapo pichani). Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Frank Mvungi-Maelezo
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) imeteketeza vipodozi visivyofaa kwa
matumizi ya binadamu vyenye thamani ya takribani Shilingi Milioni 188 katika
kipindi cha mwaka 2012/2013.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Gaudensia Simwanza
wakati akizunguza na wanahabari kwenye mkutano na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Alisema TFDA imeweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia
njia mbalimbali ambazo ni pamoja na usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya
biashara ya bidhaa husika na ukaguzi wa majengo ya vipodozi.
Simwanza aliongeza kuwa hatua nyingine ni ufuatiliaji wa vipodozi katika soko
ili kujiridhisha kuwa vina ubora na usalama unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na
taratibu zilizowekwa.
Alibainisha kuwa vipodozi ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu vina
madhara kama vile kusababisha kupata mzio wa ngozi, kusababisha ugonjwa wa
ngozi kwa mtumiaji.
“Matumizi ya vipodozi vyenye viambata vya zebaki (mercury) kwa mama
wajawazito huathiri mtoto tumboni hali inayoweza kusababisha madhara makubwa
kwa mtoto atakayezaliwa.
Alifafanua zaidi kuwa viambato kama Zirconium na Vinyl Chloride husababisha
kansa ya ngozi na mapafu kwa mtumiaji wa vipodozi vyenye kemikali.
Simwanza alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kuacha matumizi ya
vipodozi vyenye viambata vyenye sumu na kemikali.
TFDA imekuwa ikifanya operesheni na ukaguzi wa vipodizi katika maduka
mbalimbali yanayouza bidhaa hizo na kukamata bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya
binadamu na kuziteketeza kwa mujibu wa sheria.
ReplyDelete-Ngozi ya kughushi!,
-Makucha ya kughushi!,
-Kope za kuhgushi!,
-Makalio ya kughushi!,
-Manyonyo ya kughushi!,
-Mikogo ya kutembea ya kughushi!,
-Mikogo ktk maongezi ya simu ya kuhgushi!,
-Mapozi ktk picha ya kughushi!,
Kila kitu cha kughushi!
-Tabasamu nalo litakuwa la kughushi?
Eeehhhh, ni balaa!
Mnaotumia Sindano za kukuza unene na makalio mtakuja dunga zilizokwisha eksipaya mkanenepa kama tembo na msirudi tena kawaida, shauli zenu TFDA imechakza mzigo mbovu inawasaidia.
Urembo wa kughushi utawachuna ngozi wa akina mama na akina dada Tanzania!
Wanawake mujifunze kujiamini katika uhalisia kama mlivyo!
Hivi vipodozi vichomwe ili iwe funzo kwa kina dada wasioridhika rangi yao nzuri.
ReplyDelete