WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo wametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaojulikana kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. 

Ujenzi huo wa mji wa kisasa ambao utakuwa na nyumba za kuishi za kisasa za watu wa kipato cha kati unajumuisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 7,000 zikiwa na huduma zote za kujamii eneo moja. Akizungumzia mradi huo mkubwa unaotekelezwa kati ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni ya Azimio, Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo aliwaeleza wajumbe wa Bodi ya shirika hilo kuwa ujenzi wa makazi hayo ya kisasa kwa wananchi wa kipato cha kati unaendelea vizuri.

 Alisema eneo hilo litakuwa na nyumba bora na za kisasa zikiwa na huduma zote za msingi kwa jamii kama maduka, shule, hospitali, masoko, viwanja vya michezi, kituo cha polisi, kituo cha zimamoto, eneo la ujenzi wa majengo ya ibada, majengo ya burudani pamoja na miundombinu ya kisasa ya maji safi na maji taka.

 Alisema ujenzi wa mradi huo wa kisasa utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua watu takribani elfu 30 ambao watapata makazi bora nay a kisasa katika eneo hilo la Kigamboni. Akifafanua zaidi Mhandisi Msemo alisema ujenzi wa nyumba hizo utakuwa na awamu tatu; ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwaka 2016 ikiwa na nyumba 2,500, huku awamu ya pili ya ujenzi itakamilika 2017 ikiwa na nyumba bora na za kisasa 2,500.

 “…Awamu ya tatu tunatarajia ikamilike mwaka 2018 hii itakuwa na nyumba 2,460,” alisema Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Msemo akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari juu ya mradi huo. Aidha akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Ramadhan Dau alisema nyumba zote zitakazojengwa katika mradi huo zitauzwa kwa watu wenye kipato cha kati watakaohitaji.

 Alisema zipo zitakazouzwa kwa fedha taslimu na nyingine kwa makubaliano ya mikopo kadri ya utaratibu utakavyotolewa na shirika hilo pamoja na mwekezaji walieshirikiana naye kutekeleza mradi huo, yaani kampuni ya Azimio.

 Alisema bei ya nyumba moja inakadiriwa kuuzwa kuanzia dola za Kimarekani elfu 80 hadi 130, na tayari wameanza kupokea fedha na maombi kwa watakaohitaji au kulipa kidogo kidogo kwa utaratibu utakao kubalika. Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa bodi walipongeza juhudi za uongozi wa NSSF kwa kubuni mradi huo wa kisasa ambao utawasaidia wengi na hivyo kushauri kuna haja ya kutekelezwa na mikoa mingine. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa Dege ECO Village wa Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu akifuatilia. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa Dege ECO Village wa Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu akifuatilia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. The mdudu,mm nashindwa kuelewa kabisa hivi hapo ni Tanzania yetu na Shilingi yetu au tuko UNITED STATE OF AMERICA? Hii kitu inanikera sn huyo mwenye kanzu msicheke nae mwekeni uso wa ukauzu au uso wa simba ili tuiokoe Shilingi yetu coz hao ndio wanaoididimiza chini Shilingi yetu them they dont care but Dr Dau u have no choice lazima uiokoe Shilingi ili uchumi wetu ukae imara kwa pesa yetu ya nchi JAMANI NDUGU ZANGU WATANZANIA inafu is inafu sote kwa pamoja tuseme DOLA BASI,sio watu wachache tena wasiokua na uchungu na watt wetu na taifa letu kwa ujumla watubuluze wanavyo taka,by the mdudu anaekerwa na DOLA hapo Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...