Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa amepokea zawadi yenye heshima kwa asili ya watu wa korea kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Jamhuri ya Korea Mr. AHN Hong  Joon (kushoto) kiongozi huyo na ujumbe kutoka Bunge la Korea na shirika la kimataifa la misaada la Korea-KOICA katikati ya wiki  walimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ofisini kwake kuzungumzia masuala ya mashirikiano na maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (kulia) akielezea fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Dodoma kwa ujumbe wa bunge la korea wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge hilo Mr. AHN Hong Joon (wa pili kulia), ujumbe huo wa bunge la korea katikati ya wiki ulimtembelea Mkuu wa Mkoa Dodoma kuzungumzia masuala ya mashirikiano na maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akiwa na ujumbe kutoka Bunge la Jamhuri ya Korea wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje ya bunge la Korea Mr. AHN Hong Joon (mwenye tai nyekundu waliokaa), ujumbe huo kutoka Korea ulimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma katikati ya wiki na kuzungumzia masuala ya mashirikiano na maendeleo. PICHA NA JEREMIA MWAKYOMA WA OFISI YA MKUU WA MKOA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...