Baadhi ya wafanyakazi wanawake  wa Benki ya NBC wakibeba gunia la unga tayari kwenda kutoa msaada kwa wagonjwa wanawake waliolazwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na kuwajali wanawake wenzao walio katika shida. 
Mmoja wa maofisa waandamizi wa Benki ya NBC, Sarah Laizer , akikabidhi  jora la khanga kwa Msaidizi wa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya  Kansa ya Ocean Road, Sr. Genoviva Mlawa  (kushoto) pamoja na vitu vingine vilivyotolewa na wanawake hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Baadhi ya wafanyakazi wanawake hao wakiandaa khanga tayari  kwenda kuwakabidhi wagonjuwa wanawake waliolazwa katika hospitali hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake  wa Benki ya NBC,  wakipiga picha pamoja na Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Ocean Road , Dar es Salaam walipokwenda kuwatembelea wagonjwa wanawake waliolazwa katika hospitali hiyo na kuwapa aina mbalimbali za misaada kama sehemu ya maadhimisho aya Siku ya Kimataifa ya Wanawake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Haikuwa Dar es Salaam pekee kwani hapa wafanyakazi wa Benki ya NBC Mkoani Singida nao walitembelea katika Hospitali ya mkoa huo na kwenda kutoa aina mbalimbali za misaada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Binafsi nimeanza kutambua uwepo wa siku hii kwa mara ya kwanza 2004 nilipoanza kuishi Ulaya kutokana na jinsi ilivyokua ikipewa nafasi na thamani kwa wenyeji,licha ya nafasi na thamani hiyo mara nyingi zawadi kwa walengwa zilihusisha mtu na mtuwe yaani kumpa ua,kumtoa out na kutakiana salam za heri ngazi ya familia au rafiki wa karibu, hii ina akisi zaidi aina ya maisha ya wenzetu.Nimeguswa na nimependezwa mno jinsi sherehe hizi zilivyofanikishwa nyumbani, nasi pia tumeziendesha kivyetuvyetu kwa kuakisi staili yetu ya kiafrika zaidi(upendo na kujaliana).Nimeona akina dada Shamimu, hawa wa NBC nao..ni vizuri kwa staili kama hii kwa wakati ujao tukawaangalia pia wale wa vijijini kwa kuwafariji,wengi wao wapo ktk hali ngumu.Nawapa hongera wote kwa mazuri mliyoyafanya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...