Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo amesema wazazi kwa kushirikiana na walimu wanayo nafasi kubwa katika kuhakikisha elimu Wilayani Chato inaboreka.
Ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa elimu Wilayani Chato kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halamshauri hiyo.
Mhe. Mpogolo amesema si muda muafaka sasa wa kumwachia mwalimu kuhusu masuala yote ya elimu bali kila mtu hasa mzazi anayo nafasi kubwa ya kuhakikisha mtoto anapata mahitaji yote ya kielimu.
“Maadili ya mtoto yanaanzaia ngazi ya familia ambapo kuna wazazi au walezi , mzazi akikaa pembeni akikaa pembeni akitegemea mwalimu atafundisha kila kitu sio vizuri hata kidogo” alisisitiza mkuu wa Wilaya.
Kwa upande wao wadau wa elimu Wilayani Chato yakiwemo mashirika na taasisi zisizo za kiserikali zinazoshirikiana na Halmashauri ya Chato katika kutoa huduma za kijamii ikiwemo elimu wameitaka serikali kuboresha miundombinu ya shule pamoja na kufanya kazi kwa karibu na taasisi hizo ili kuboresha hali ya elimu Wilayani Chato.
Bibi Stella Maganga kutoka shirika lisilo la kiserikali la RUDDO lenye makao makuu yake wilayani Biharamulo ambalo husomesha watoto wasio na uwezo waliopo Chato alisitiza umuhimu wa serikali kushirikiana na Taasisi hizo kwani serikali peke yake haiwezi kuleta maendeleo pasipo kushirikiana na sekta binafsi.
Wadau wengine waliochangia katika kikao hicho cha wadau walitaka serikali kuboresha idara ya ukaguzi wa Shule kwa kuwapa mahitaji muhimu ili waweze kutimiza majukumu yao.
Wadau wengine walichangia umuhimu wa watoto kupata chakula wakiwa shuleni ili waweze kumudu masomo hayo kwa muda wote wawapo shule.
Akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya aliwataka wadau hao wawe na azimio la pamoja la kuinua kiwango cha elimu kwa kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2014 kutoka nafasi ya 3 kimkoa hadi nafasi ya kwanza.
Wilaya ya Chato inazo shule za msingi 131 kati ya hizo 3 ni za binafsi,na shule 24 za sekondari ambapo ufaulu wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2013 ulikuwa ni wa asilimia 58 ukilinganisha na mwaka 2012 ulikuwa ni wa asilimia 41 na mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013 ufaulu ulikuwa wa asilimia 55 ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo ufaulu ulikuwa wa asilimia 44, kwa kidato cha tano na sita kwa mwaka 2013 ufaulu ulikuwa wa asilia 99 ukilinganisha na asilimia 97 kwa mwaka 2012.
Kaimu
Mkuu wa idara ya Elimu Bw. Isdori Kazaura akitoa taarifa ya Elimu kwenye kikao
hicho cha wadau wa elimu
Mkuu wa Wilaya y a Chato Mhe. Rodrick
Mpogolo (wa kwanza kushoto ) akishiriki katika majadiliano kwenye kikundi ya
namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za elimu Wilayani Chato
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chato ndg.
Ibrahim Bagura (wa pili kutoka kulia ) akishiriki katika majadiliano kwenye
kikundi ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za elimu Wilayani
Chato
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...