Nilimsaidia usafiri dada mmoja,siku ya ijumaa wiki jana, Dada huyo alikuwa anatokea maeneo ya Tuangoma kuelekea maeneo ya Keko.Nilimshusha JKT Mgulani. Bahati mbaya alisahau simu yake kwenye gari. Simu hiyo iliishiwa chaji muda mchache baada ya kuisahau kwenye gari langu. Mie nikaichukua na kuiweka  kwenye chaji kama masaa mawili hivi. 
Nilipoiwasha nilikuta keshafunga kadi yake na sijaweza hata kutafuta namba za watu wanaomjua ili niwasiliane naye. Pia hata jina sikuwahi kumuuliza.
Naomba kama dada huyo atasoma tangazo hili au mtu yeyote anamfahamu dada aliyepotelewa na simu yake anipigie kwa namba 0755877827.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Watu wote ngekuwa kama wewe hiyo nchi ingeendelea hongera kaka....wabongo wanatakiwa kuchukua mfano...cha mtu mavi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Is this real? U a the only one left, 5 like u wiped change bongo!

      Delete
  2. Kwa moyo kama huo wa kujali cha mtu ,endelea nao tu kaka,na nakutabiria kuingia peponi kwa mlango uutakao.

    ReplyDelete
  3. Aron MsigwaApril 14, 2014

    Hongera kwa moyo wa upendo uliouonyesha!ushauri wangu kwako tafuta line nyingine au kama una line unayoitumia wewe mwenyewe unaweza kuiweka kwenye simu hiyo iliyoachwa yamkini kuna majina yaliyohifadhiwa kwenye phone memory ikawa rahisi kuyaona maana yatakuwa tofauti na yale uliyoyahifadhi wewe kukuwezesha kuwatafuta ndugu jamaa na marafiki kuliko kuendelea kutumia line hiyo iliyofungwa.

    ReplyDelete
  4. Hongera ndugu kwakuwa na utu.

    ReplyDelete
  5. May Allah Reward u for this!!

    ReplyDelete
  6. ww wa peponi kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...