Nilimsaidia usafiri dada mmoja,siku ya ijumaa wiki jana, Dada huyo alikuwa anatokea maeneo ya Tuangoma kuelekea maeneo ya Keko.Nilimshusha JKT Mgulani. Bahati mbaya alisahau simu yake kwenye gari. Simu hiyo iliishiwa chaji muda mchache baada ya kuisahau kwenye gari langu. Mie nikaichukua na kuiweka kwenye chaji kama masaa mawili hivi.
Nilipoiwasha nilikuta keshafunga kadi yake na sijaweza hata kutafuta namba za watu wanaomjua ili niwasiliane naye. Pia hata jina sikuwahi kumuuliza.
Naomba kama dada huyo atasoma tangazo hili au mtu yeyote anamfahamu dada aliyepotelewa na simu yake anipigie kwa namba 0755877827.
Watu wote ngekuwa kama wewe hiyo nchi ingeendelea hongera kaka....wabongo wanatakiwa kuchukua mfano...cha mtu mavi
ReplyDeleteIs this real? U a the only one left, 5 like u wiped change bongo!
DeleteKwa moyo kama huo wa kujali cha mtu ,endelea nao tu kaka,na nakutabiria kuingia peponi kwa mlango uutakao.
ReplyDeleteHongera kwa moyo wa upendo uliouonyesha!ushauri wangu kwako tafuta line nyingine au kama una line unayoitumia wewe mwenyewe unaweza kuiweka kwenye simu hiyo iliyoachwa yamkini kuna majina yaliyohifadhiwa kwenye phone memory ikawa rahisi kuyaona maana yatakuwa tofauti na yale uliyoyahifadhi wewe kukuwezesha kuwatafuta ndugu jamaa na marafiki kuliko kuendelea kutumia line hiyo iliyofungwa.
ReplyDeleteHongera ndugu kwakuwa na utu.
ReplyDeleteMay Allah Reward u for this!!
ReplyDeleteww wa peponi kabisa.
ReplyDelete