SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YAFANA MJINI ROMA

Watanzania nchini Italia, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014, walikutana mjini Roma kwenye ukumbi wa Ubalozi uliopo Viale Cortina d’Ampezzo 185, kusherehekea sikukuu ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Dkt. James A. Msekela. Sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania Italia, Maofisa wa Ubalozi na familia zao, Maofisa wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Roma na familia zao pamoja na Watanzania waishio Italia. 
                               Keki yetu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 
       Bi. Mary Mtemahanji, mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzani Modena akiimba kwa  furaha wakati wa kufungua champeign.
                   Bi. Zainab na Bw.Peter wakikata keki ya Muungano kwa pamoja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizi keki za ughaibuni kwa kweli zimepambwa vizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...