SHEREHE YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YAFANA MJINI ROMA
Watanzania nchini Italia, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014, walikutana mjini Roma kwenye ukumbi wa Ubalozi uliopo Viale Cortina d’Ampezzo 185, kusherehekea sikukuu ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Dkt. James A. Msekela. Sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania Italia, Maofisa wa Ubalozi na familia zao, Maofisa wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Roma na familia zao pamoja na Watanzania waishio Italia.
Bi. Mary Mtemahanji, mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzani Modena akiimba kwa furaha wakati wa kufungua champeign.
Bi. Zainab na Bw.Peter wakikata keki ya Muungano kwa pamoja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Hizi keki za ughaibuni kwa kweli zimepambwa vizuri.
ReplyDelete