Afisa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Frank Shija akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani
 
 Mwenyekiti wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza Alfat Mansoor (Dogo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jijini Dar es Salaam.
 Mchezaji aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania kuibuka mabingwa wa Dunia kw kufunga magoli matatu kwa mojadhidi ya Burundi Frank William(mwenye kofia nyekundu) akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake mara baada ya juwasili airport,kushoto ni Hassan Jaffar,Emmanuel Amos, na Hassan Seleman.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda akiwa amebeba kombe la ubingwa dunia mara baada ya kupokea timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu kutoka Burundi jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya saa 9:35 mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka.
Wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania ilyo nyakuwa ubingwa wa dunia katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapa katika mashindano hayo. Picha na Frank Shija - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera Tanzania!!!!

    Kikwete oyeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  2. Jezi yaop kali sana Bluuuuu !

    (Ankali na watu wako wa Liverpool na Man U msije kmasema ohhh Chelsea, hiyo ni Tanzania)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...