Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa.
Baadhi
ya Wanachama wapya wapato 300 kutoka kata ya Ilemba, waliojiunga na
chama cha CCM,wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho
na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.
Sehemu ya bweni hilo la Wasichana,ujenzi wake ukiendelea.kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Bwa.Abeid
Missana,amesema Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 237 inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya
Sayansi,Nyumba za walimu na idadi ya waalimu waliopo.
Kinana akipitishwa kukagua ujenzi wa zahanati hiyo na Ofisa Mtendaji wa Kijiji,Kata ya Ilemba,Bwa.Desdei Kayola (pichani kati)
Muonekano
wa ujenzi wa kituo hicho cha afya,kata ya Ilemba ambacho kikikamilika
kitaokoa maisha ya idadi kubwa ya watu,ambayo inapotea kutokana na uduni
wa huduma ya afya iliyopo sasa,hivyo kituo hicho kitatatua changamoto
zilizopo za huduma ya afya.
Kinana
akishiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga
Vijijini. Ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi
wa kituo hicho
Wananchi wa kijiji cha Ilango,Kata ya Ilemba,Sumbawanga vijijini wakimpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa aina yake alipokuwa akiwasili kijijini hapo ambapo pia aliongea na kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo na kuyafanyia kazi.
hizi ndizo siasa tunazozitaka sio siasa za kupandikiza chuki kwa wananchi - tunataka maendeleo sio porojo!
ReplyDelete