Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa.
Baadhi ya Wanachama wapya wapato 300 kutoka kata ya Ilemba, waliojiunga na chama cha CCM,wakila kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.
Sehemu ya bweni hilo la Wasichana,ujenzi wake ukiendelea.kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini,Bwa.Abeid Missana,amesema Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 237 inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya Sayansi,Nyumba za walimu na idadi ya waalimu waliopo.
Kinana akipitishwa kukagua ujenzi wa zahanati hiyo na Ofisa Mtendaji wa Kijiji,Kata ya  Ilemba,Bwa.Desdei Kayola (pichani kati)
Muonekano wa ujenzi wa kituo hicho cha afya,kata ya Ilemba ambacho kikikamilika kitaokoa maisha ya idadi kubwa ya watu,ambayo inapotea kutokana na uduni wa huduma ya afya iliyopo sasa,hivyo kituo hicho kitatatua changamoto zilizopo za huduma ya afya.
 Kinana akishiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi wa kituo hicho

Wananchi wa kijiji cha Ilango,Kata ya Ilemba,Sumbawanga vijijini wakimpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa aina yake alipokuwa akiwasili kijijini hapo ambapo pia aliongea na kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo na kuyafanyia kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hizi ndizo siasa tunazozitaka sio siasa za kupandikiza chuki kwa wananchi - tunataka maendeleo sio porojo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...