Marehemu Adam Kuambiana enzi za uhai
wake.
MWIGIZAJI
na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati
akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa
matibabu alfajiri ya leo.
Habari zinasema Marehemu
alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa
Remmy, Dar es salaam.
Kabla ya mauti kumfika, Adam
alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.
Globu ya Jamii inaungana na
familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa Bongo Movie katika
kuomboleza kifo cha nyota huyu wa filamu.
Mola aiweke roho ya marehemu
mahala pema Peponi
AMINA
jamani hili tumbo la siku hizi mpaka linatuletea mauti ni nini?Amina ngaluma nae alikuwa analalamika tumbo tumbo mpaka mauti imemchukua,Mungu tunusuru.
ReplyDeleteNimesikitika sana na kikubwa zaidi ni ile kupuuzia na kupotezea magonjwa yanapoanza. Ni vema tuwe tunaenda kuchekiwa mara kwa mara haswa chochote kinachohusu damu, iwe kutapika, kukohoa, hata choo. Nimeshaumwa na nyoka nikapona kwa rehema ya Mungu sasa nikiona na mwingine amepatwa na janga hili tuwe macho kwa kweli. Alikuwa na kipaji cha pekee
ReplyDelete