Mkurugenzi wa MasokoUtafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Jimbo la Hai kwa ajili ya ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT jimbo la Hai. Katika harambee hiyo Benki ya CRDB ilitoa shilingi milioni 20 kufanikisha ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
Baadhi ya waumini wakiingia kanisani wakati wa ibada maalumu ya iliyofanyika katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai, iliyokwenda sambasamba na harambee ya kuchangia kanisa hilo pamoja na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...