Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga ametembelea kivuko cha Kiyungi kinachofahamika kama daraja la Mnepo kinachounganisha wilaya ya Hai na Moshi ambacho sasa hivi kipo katika hali mbaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Mhe Makunga ameahidi kwamba kivuko hicho kitaanza kufanyiwa ukarabati wa dhararu Jumamosi ijayo angalau kiweze kutumika wakati zinasubiriwa fedha za ujenzi wa kivuko kipya.Ameeleza kuwa kampuni ya Sukari ya TPC imekubali kutoa baadhi ya vifaa vya ukarabati.
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga(Katikati) akiwa na Afisa mtendaji mkuu wa kiwanda cha TPC,,Jaffari Ally(Mbele) na diwani wa kata ya Machame Weruweru,Adris Mandrai wakikagua daraja la Mnepo la Kiyungi.
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga(aliyekunja mikono kifuani) akijadili jambo kwa pamoja na viongozi wa kata ya Weruweru,kiwanda na TPC na wahandisi wa ujenzi jinsi ya kukarabati daraja la mnepo la Kiyungi.
Mhe Makunga na ujumbe wake wakishuhudia jinsi wananchi wanavyovuka mto kwa kutumia kivuko cha mnepo cha Kiyungi.
Diwani wa kata ya Machame Weruweru Adris Mandrai akipita katika kivuko cha mnepo cha Kiyungi
Wananchi wakiendelea kuvuka kivuko hicho cha Mnepo
Viongozi na wataalamu wakijadili jinsi ya kuimarisha kivuko cha Mnepo cha Kiyungi (Picha zote na Richard Mwangulube)
Nimekipenda hicho kivuko na watumiaji wake kwa sababu wanayatunza mazingira yanayowazunguka. Angalia hiyo miti na ukijani murua kabisa.
ReplyDelete