Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi (hawapo pichani) kando kando ya barabara,wakati wakielekea kwenye mkutano hadhara uliofanyika katika uwanja wa People's mjini Singida,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye na viongozi wengine mbalimbali chama.
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wakati akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa People's mjini Singida jioni hii,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Mwigulu Nchemba na viongozi wengine mbalimbali wa chama.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,na Mbunge wa jimbo la Iramba Mashariki,Mh Mwigulu Nchemba akiwa kwenye moja ya piki piki kwenye matembezi ya kuelekea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa People's mjini Singida,ambaoo wananchi wamejitokeza kwa wingi.

Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa mji wa Singida jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa People's mjini Singida.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikad,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya siku nane mkoani humo ya Kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.

 Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa mji wa Singida jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa People's mjini Singida
 Sehemu ya Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara unaoendelea hivi sasa katika uwanja wa  People's mjini Singida,huku ukirushwa LIVE na kituo cha televisheni STAR TV.

PICHA NA MICHUZIJR-SINGIDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2014

    Mh.Kinana na ujumbe wako unatisha na mwaka ujao Chadema hawatapata kitu ila naomba nije nigombee kwenye jimbo la Ilemela nimuondoe huo mchaga wa CHADEMA na vile vile tafuta mtu atakeyemuondoa mwalimu Wenje jimbo la Nyamagana na ukiweza hayo basi CHADEMA utakuwa umeimaliza kabisa.
    Nimekuwa nafatilia safari zako mikoani na nimekubali kuwa wewe ni tishio kwa vyama vya upinzani na uchaguzi ujao watakiona cha mtemakuni pamoja na hicho wachokiita UKAWA.
    Mungu akuzidishienguvu uweze kupitia mikoa yote ya Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2014

    Ndugu, Mwigulu Nchema ni mbunge wa Iramba Magharibi sio MAshariki kama ulivyoandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...