Na  Pascal Mayalla 
 Ziara ya Meli za Jeshi la Uturuki Nchini Tanzania. Meli Nne za Kijeshi za Uturuki kwa jina la Barbaros Turkish Maritime Task Group (TMTG) zinatarajiwa kutia nanga kwa wakati mmoja katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ziara ya kijeshi ya siku 4 ambao itahusisha maonyesho ya zana za kijeshi, mazoezi ya pamoja na jeshi la wanamaji la Tanzania, huduma za kijamii na ushirikiani wa kijeshi baina ya Uturuki na Tanzania. 
Hayo yamebainishwa jiji Dar es Salaam na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovitoglu katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ubalozi wa Uturuki, jijini Dar es Salaam. 
Balozi Dovitoglu amesema lengo kuu la ziara hiyo ni kukuza ushirikiano wa kijeshe baina ya jeshi la Uturuki na majeshi ya nchi 27 za pwani barani Afrika sio tuu kuonyesha uwepo na uwezo wa kijeshi wa Jeshi la Wanamaji la Uturuki, bali pia kusaidia katika operetions mbalimbali za kijeshi barani Afrika ukiwemo vita dhidi ya uharamia kwa Pwani ya Bahari ya Hindi. 
Balozi Dovitoglu amesema meli hizo zitawasili siku ya Jumanne tarehe 27/05/2014, Siku ya Jumatano, tarehe 28/05 2014 waandishi wa habari watakaribishwa kufanya ziara katika meli hizo, baadaye wanamaji hao, watatembelea shule na kituo cha watoto yatima kugawa misaada ya kibinaadamu. 
Siku ya Alhamisi na Ijumaa, wananchi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wataruhusiwa kutembelea meli hizo kwa muda wa siku 2 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 6 mchana kujionea maonyesho ya zana za kijeshi ya Uturuki ambapo makampuni manane ya vifaa vya kijeshi ya Uturuki wataonyesha vifaa vyao. 
Makampuni hayo ni Meteksan, Otokar, TAI, Dearsan, Havelsan, Roketsan, Aselsan na STM
Meli hizo nne ni F-495 TCG kwa jina la Gediz, F-245 TCG, Oruçreis, F-511 TCG Heybeliada meli ya usindikizaji ya A-595 TCG Yarbay Kudret Güngör, zitasafiri kwa jumla ya safari ya urefu wa kilometa 30,000 katika ziara itakayochukua siku zaidi ya 100 ambapo itatembelea nchi 28 barani Afrika na kutia nanga katika bandari 40. 
 Msafara wa meli hizo, unaingia Tanzania ukitokea nchini Afrika ya Kusini, ambapo hii ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 148 iliyopita ndipo meli ya mwisho ya Uturuki ilitia nanga kwa mara ya mwisha katika Rasi ya Tumaini Jema (Cape of Good Hope) mwaka 1866. 
 Uturuki ni moja ya mataifa makubwa yenye nguvu kubwa za kijeshi la la majini, tangu enzi za utawala wa kale wa dola la Ottoman ambapo walitawala bandari nyingi barani Afrika ikiwemo miji ya Kilwa, Sofala, na Lamu kwatika Pwani ya Bahari ya Hindi. Mwisho.
 na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovitoglu katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ubalozi wa Uturuki, jijini Dar es Salaam 
na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovitoglu akihojiwa na mwandishi wa ITV Bi. Fatuma  Almasi Nyangassa  kwenye Ubalozi wa Uturuki, jijini Dar es Salaam 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2014

    chukueni utaalamu harakaharaka tulinde bara letu; wahuni wanakuja kwa kasi kutukoloni tena

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2014

    huyu fatma almasi nyangasa bado sijamuelewa,hapa kavaa hijab kama inavotakiwa,akiwa mbele ya kioo cha ITV hava hijab.hivi wanakatazwa kuvaa hijab.huko Tanganyika sijawahi kumuona mtangazaji akivaa hijab,kule Kenya wanavaa kama inavotakiwa na imani yao.hivi ni huko kwetu tu hawaruhusu ama ni wenyewe tu watangazaji?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2014

    sasa kama mtu anaamua kuvaa anavyotaka wewe inakuhusu nini? Ikiwa kinyume chake: kwenye TV akivaa hiyo hijab na kwenye maisha ya kawaida asipovaa utalalamika kwa nini anavaa hijab kwenye TV na si kwenye maisha ya kawaida? mind your own business!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2014

    mdau namba 3 hujui unachoongea,nakuacha hivyo hivyo.hiyo ni moja ya business zangu

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2014

    wewe business zako kufuatilia watu wavaa nini wakati wana baba, mama, kaka, dada zao, majirani, waajiri wao, mashere wao, mapadri wao, nk.....???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...