Na John Gagarini, Kibaha
MLINZI Bakari Mape (70) mkazi wa Mlandizi wilaya ya Kibaha mkoa wa
Pwani ameuwawa kwa kunyongwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Watu hao ambao idadi yao haikuweza kufahamika mara moja walimwua
mlinzi huyo kwa kumvunja shingo kisha kuiba kwenye duka ambalo mlinzi
huyo alikuwa akililinda.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani humo
Kamishna Mwandamizi Msaidizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio
hilo lilitokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8 usiku eneo la sokoni
Mlandizi wilayani hapa.
Kamanda Matei alisema kuwa watu hao baada ya kumwua marehemu ambaye
alikuwa akilinda duka la Conrad Masawe (53) mkazi wa Mtongani
Mlandizi, waliiba kiasi cha shilingi milioni 5.2.
"Walipomwua walingoa bati kisha kuingia ndani na kuiba fedha hizo na
kutoweka kusikofahamika huku wakimwacha marehemu hapo," alisema
Kamanda Matei.
Alisema kuwa kutokana na tukio hilo wanamshikilia mtu mmoja aitwaye
Omary Rajabu kuhusiana na suala hilo.
"Mwili wa marehemu ulikabidhiw andugu kwa ajili ya mazishi baada ya
uchunguzi wa daktari na tutawasaka watu walihusika na tukio hilo ili
mkondo wa sheria uweze kuchukua hatua kwani kitendo hicho ni ukatili
ndani ya jamii," alisema Kamanda Matei.
Aidha aliwataka wafanyabiashara waajiri watu weny umri wa kati ili
waweze kukabiliana na matukio kama hayo na kuacha kuajiri watu wenye
umri mkubwa sana kwani ni vigumu kukabiliana na matukio kama hayo.
Kamanda.....umri huo yapaswa awe anapokea pensheni kila mwezi iliaweze kujikimu maisha lakini kwakua hatuna utaratibu huo, marehemu aliamua kujituma japo kwa umri wake huo, wapo wengi sana ambao si kwa kupenda wapo ktk ajira zisizo rasmi hivyo suala la kuwashauri waajiri watazame vijana tu si ushauri sahihi kwa mtazamo wangu.Hili la kuwapa fedha za kujikimu wazee lawezekana kwakua idadi yao kwa sasa si kubwa nchini, hii ni kwa mujibu wa takwimu. ....R..I..P
ReplyDelete