Tamasha kubwa la watoto la aina yake linaloitwa ‘Extreme Kids Festival’ litafanyika katika viwanja vya
Leaders Club, Dar es Salaam, May 31 na June 1 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
Extreme Kids Festival litapambwa na michezo mbalimbali ya watoto, games, burudani pamoja na semina
fupi kwa familia.
Hili ni tamasha kubwa zaidi litakalowakutanisha watoto wengi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya
jirani kufurahia kwa pamoja michezo wanayoipenda zaidi na pia wazazi kujifunza mambo mbalimbali
kwa faida ya familia na malezi ya watoto.
Kupitia tamasha hilo, kutakuwa na vibanda mbalimbali vitakavyotoa huduma mbalimbali za familia na
wazazi watapata bidhaa bora zaidi kwa ajili ya watoto na familia nzima kwa ujumla.
Waandaaji wa Extreme Kids Festival wamesema kuwa kutakuwa na usalama wa hali ya juu kwa watoto
na wote watakaohudhuria na kwamba matumizi ya vilevi hayataruhusiwa.
Watu wazima watalipia shilingi 5,000 na watoto watalipia shilingi 3,000 tu kuingia katika tamasha hilo
Baada ya Dar es Salaam, tamasha hilo litafanyika pia mwaka huu jijini Arusha, October 4 na October 5,
Mt. Meru Hotel Gardens na jijini Mwanza December 6 na December 7 katika uwanja wa Nyamagana.
Hili ni tamasha la kihistoria litakalompa mtoto kilicho bora zaidi na kumpa sababu nyingi zaidi za
kufurahi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...