Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 62 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka Jumapili ya leo katika barabara ya Thika, ambayo ni moja ya njia kuu zenye magari mengi jijini Nairobi, Kenya.Majeruhi 20 kati ya hao wako mahututi.

Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya Bw. Moses Ombati amenukuliwa akisema kuwa  mabomu hayo yamelipuka kwenye mabasi ya abiria mawili tofauti, ambapo Naibu Mkuu wa kitengo cha kutengua Mabomu, Bw, Eliud Lagat amesema milipuko hiyo imetokana na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.

Milipuko hiyo na maafa hayo yamekuja siku moja baada ya watu wanne kuuwawa kwa mlipuko wa bomu ya kutupwa kwa mkono katika kituo cha mabasi mjini Mombasa. Mlipuko mwingine katika ufukwe wa bahari haukuleta madhara.


Kenya imekumbwa na wimbi la mashambulio ya bunduki na milipuko ya mabomu toka nchi hiyo ilipopeleka majeshi yake kupambana na wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al-Shabab mwaka 2011, ambao wameapa kuendeleza mashambulio ya kigaidi kama kulipiza kisasi kwa kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    Get back from Somali pls.
    Don't kill Kenyan cause of white man money!
    Hata white man alishindwa huko na kuondoa, waachieni Matatizo yao, ah yeye mkubwa aende tena Sio kuua wakenya wasio na hatia. Don't be puppet kenya government .

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2014

    Poleni Wakenya. Ugaidi si mzuri kwa nchi yoyote unaleta woga kwa raia na kutishia maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...