Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 62
kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka Jumapili ya leo katika barabara ya
Thika, ambayo ni moja ya njia kuu zenye magari mengi jijini Nairobi, Kenya.Majeruhi
20 kati ya hao wako mahututi.
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya Bw. Moses Ombati amenukuliwa
akisema kuwa mabomu hayo yamelipuka
kwenye mabasi ya abiria mawili tofauti, ambapo Naibu Mkuu wa kitengo cha
kutengua Mabomu, Bw, Eliud Lagat amesema milipuko hiyo imetokana na mabomu
yaliyotengenezwa kienyeji.
Milipuko
hiyo na maafa hayo yamekuja siku moja baada ya watu wanne kuuwawa kwa mlipuko wa
bomu ya kutupwa kwa mkono katika kituo cha mabasi mjini Mombasa. Mlipuko
mwingine katika ufukwe wa bahari haukuleta madhara.
Kenya
imekumbwa na wimbi la mashambulio ya bunduki na milipuko ya mabomu toka nchi
hiyo ilipopeleka majeshi yake kupambana na wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la
kigaidi la Al-Shabab mwaka 2011, ambao wameapa kuendeleza mashambulio ya
kigaidi kama kulipiza kisasi kwa kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia.
Get back from Somali pls.
ReplyDeleteDon't kill Kenyan cause of white man money!
Hata white man alishindwa huko na kuondoa, waachieni Matatizo yao, ah yeye mkubwa aende tena Sio kuua wakenya wasio na hatia. Don't be puppet kenya government .
Poleni Wakenya. Ugaidi si mzuri kwa nchi yoyote unaleta woga kwa raia na kutishia maisha ya wananchi wasiokuwa na hatia.
ReplyDelete