Mjumbe wa Kamati ya Urasimishaji wa Kazi za wasanii wa Filamu na Muziki hapa nchini ambaye pia ni Afisa kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Wilhad Tairo akifafanua jambo kwa mfanyabiashara wa duka la Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Bidhaa zisizo kuwa na Stempu za TRA, Operesheni hiyo ya wiki mbili iliyoanza jana jijini Dar es Salaaminatekelezwa kwa uhirikiano wa TRA, Bodi ya Filamu, Basata na Cosota
Mfanyabiashara wa duka CDs za Filamu lililopo maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam akieleza jambo kwa maafisa wa Kikosi kazi kwa ajili yakukagua bidhaa ambazo azizingatii taratibu kabla ya kuingizwa sokoni leo jijini Dar es Salaam.
Muuzaji wa duka la CD za Filamu katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam akiwaonyesha Stempu za TRA katika CD zake wakaguzi kutoka TRA,Bodi ya Fila, Basata na Costa ambao walifika dukani kwake kwa ajili ya ukaguzi wa bidhaa ambazo zimeingizwa sokoni bila kufuata taratibu za kisheria iliwemo kuweka Stika za TRA kama sheria inavyotaka.Kamati ya urasimishaji wa kazi za wasanii wa Filamu na Muziki wameanza Operesheni ya wiki mbili katika jiji la Dar es Salaam ili kuleta ufanisi katika mapato ya Wasanii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...