Mamia ya wapenzi na washabiki wa klabu kongwe ya mpira wa miguu hapa nchini Simba leo mchana wamejikusanya kwa wingi katika makao makuu ya klabu yao hiyo,kupinga Michael Wambura kuondolewa kwenye orodha ya wagombea kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.Wanachama hao ambao walizunguka jengo hilo na kutaka wapewe sababu za msingi kwanini Wambura ameondolewa huku wakitaka kufanya vurugu lakini vyombo vya usalama waliwahi kufika eneo la tukio na kuweza kuwatuliza wanachama Hao.
 Polisi wakiwa wamefika eneo la klabu ya simba ili kuimarisha ulinzi na kuwataka wanachama wa simba kutulia ili wapate majibu kwa kamati ya uchaguzi.
 Wanachama wa simba wakiwa wamelizunguka Jengo la klabu yao mchana huu kupinga kuondolewa kwa wambura kwenye uchaguzi wa klabu hiyo.Picha na Sek David

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 29, 2014


    Duh...kweli mmewezwa...kero zote za maji, usafiri, foleni, bei juu,wizi mkubwa na mdogo,mbwa mwitu na mengineyo .......wala hayawasumbui...ila hili la ....mshikiki...ama kweli wamepuliziwa moshi wa kijiti...hahahaha....

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 29, 2014

    BURUDANI AMANI,SIASA MACHAFUKO. WEE WA KWANZA VP BWANA KILA KITU UNALETA SIASA. NANI KAKUAMBIA MATATIZO YAKO YANAMALIZWA NA WANASIASA?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 29, 2014

    Hoja ya msingi ni kama alikwenda mahakamani, kama ni hivyo adhabu yake inajulikana. Mambo mengine ni kuleta siasa ktk mpira.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2014

    maneno maneno tu... mbona wengine mpaka jela wakaenda na bado mkawachagua. acheni chuki binafsi mpeni nafasi wambura angalau aenguliwe kwenye kura na si vinginevyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...