Wito umetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwaimu kwa jamii ya Umma wa Tanzania kutunza ardhi na udongo kwa ajili ya matumizi endelevu na kuifanya ardhi iwe na uwezo wa kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo na kutoa huduma zingine muhimu ili kuepuka hali ya jangwa na ukame kwa kizazi cha sasa na kijacho na pia kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. 

Mheshimiwa Mwalimu amesema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani. Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika katika kijiji cha Mabilioni tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.

 Aliongeza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa robo ya dunia ambayo ni zaidi ya hekta bilioni 3.6 inatishiwa na janga la kuenea kwa hali ya ukame na jangwa. Hivyo basi alisema ni wajibu wa kila mmoja kulinda ardhi ili iweze kuleta manufaa baadaye sababu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunasababisha matatizo ya kiuchumi,kimazingira na kijamii . 

Vivyo hivyo kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunapelekea ardhi kupunguza uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula na kuongeza umaskini . 

Mwisho alitoa wito kwa Hamashauri zote Nchini kuunda kamati za Mazingira kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Wilaya. Pia aliomba vyombo vya habari Nchini kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuchukua njia thabiti za kupambana na kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni Ardhi ni mustakabali wa maisha, tuilinde dhidi ya uharibifu.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Same Mheshimiwa Henry Kapufi wakisikiliza maelekezo juu ya ufugaji nyuki kutoka kwa mmoja wa wafugaji(hayupo pichani) katika kijiji cha mabilioni wilayani Same katika siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipanda mti wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa duniani zilizofanyika katika kijiji cha mabilioni wiayani Same.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akiongea na wananchi katika maadhimisho hayo .
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akicheza ngoma ya msanja sanjari na kikundi cha wakinamama wa kijiji cha mabilioni wilayani Same katika maadhimisho ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akihutubia katika siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani. Kitaifa maadhimisho ya siku hiyo yamefanyika katika kijiji cha mabilioni Tarafa ya Hedaru wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.
Sehemu ya umati wa Wananchi waliojitokeza katika kuadhimisha siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame duniani iliyofanyika kitaifa katika kijiji cha mabilioni wilayani Same mkoa wa Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2014

    Tupande miti, hata tunahitaji programmu za kuhamasisha kupanda miti kwenye ardhi binafsi. Na tuwe pia na upandaji miti kwenye maeneo ya umma. Ikiwezekana kila mti uwe na thamani kama shilingi elfu mbili, ili hii pia itengeneze ajira na motisha ya kuongeza maeneo yenye misitu ya miti asilia kwa vizazi vijavyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...