Uchunguzi umeanza asubuhi hiikujua chanzo cha kuzuka kwa moto karibu na hostel za wasichana katika skuli ya sanaa na lugha (School of Humanities) katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) usiku wa kuamkia leo. Athari za moto huo bado hazijajulikana.
Wakaazi wa mji huo walisikia vingo'ra vya magari ya zimamoto yakielekea chuoni huko kwa kasi, na miali mikubwa ya moto kuonekana katika vilima vya Chimwaga kipo chuo hicho usiku wa manane. Taarifa zaidi tutapeana kadiri zitavyotufikia
badala ya kusaidia kuokoa kinachowezekana, wanakomaa kurekodi tukio, hao ndioyo wasomi wa bongo
ReplyDeletehii tabia imekithiri sana bongo yetu watu badala ya kutoa msaada baada ya majanga wanakimbilia kupiga picha tu na kushare mitandaoni.jirekebisheni vijana
ReplyDeleteKwani fire extinguisher zipo?, na zimamoto wako wapi mpaka muweke vijana wetu kwenye kuzima moto..Hiki chuo kipya sana tuombe tusiingie hasara ya kukijenga tena. Kiusalama afadhali tu wapige picha huu siyo moto wa kuzima kwa ndoo za maji au mchanga ni moto mkubwa.
ReplyDeleteAshukuriwe mungu coz students were ok, na it was hard time kwao coz they'r in final exams (UE)
ReplyDelete