MOJA ya vitu ambavyo wazanzibari watakumbuka ni jinsi kundi la Kenya ambalo hivi karibuni liliibuka kundi bora katika MTV Base lilivyovamia jukwaa na kuendesha shoo ya saa moja na nusu iliyokuwa na uhakika.
Kundi hilo lenye watu watano wakiongozwa na mtia sauti Bien Baraza liliwaacha hoi wazanzibari waliofurika katika ukumbi wa Mambo uliopo ndani ya Ngome Kongwe na muziki wenye mahadhi ya Afro Pop.
Muziki huo ambao uliwateka vijana kutokana na midundo yake na maneno ya kuchombeza ulionesha kwanini MTV Base walisema ni kundi bora.
DSC_0134
Wanamuziki wa Bendi ya Sauti Sol kutoka nchini Kenya likiwasha moto kwenye tamasha la ZIFF 2014 usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar. Pichani ni Bien Baraza (vocalist) na Willis Austin Chimano (vocalist) wakifanya yao jukwaani. (Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).
DSC_0163
Bien Baraza (kushoto) na Willis Austin Chimano (kulia) wakitoa burudani kwenye jukwaa la ZIFF 2014.
DSC_0193
Polycarp Otieno (Quitar & Vocalist) akifanya yake ndani ya ZIFF 2014.Sauti Sol watikisa tamasha la ZIFF 2014

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2014

    Hivi mbona baadhi ya wasanii wakati mwingine hawavai nguo za kuwasitiri mwili vizuri? mmeshajiuliza?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2014

    mm nshajiuliza sana.kwanini wanaume utakuta wanavaa suti ama nguo nyengine za kusitiri miili yao vyema,ukija kwa kina dada wameziba chuchu na sehemu ndogo ya kiuno then wanasema wanadhalilishwa.mdau wa hapo juu hii ni kazi ya shetani.nshakujibu swali lako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...