MOJA ya vitu ambavyo wazanzibari watakumbuka ni jinsi kundi la Kenya ambalo hivi karibuni liliibuka kundi bora katika MTV Base lilivyovamia jukwaa na kuendesha shoo ya saa moja na nusu iliyokuwa na uhakika.
Kundi hilo lenye watu watano wakiongozwa na mtia sauti Bien Baraza liliwaacha hoi wazanzibari waliofurika katika ukumbi wa Mambo uliopo ndani ya Ngome Kongwe na muziki wenye mahadhi ya Afro Pop.
Muziki huo ambao uliwateka vijana kutokana na midundo yake na maneno ya kuchombeza ulionesha kwanini MTV Base walisema ni kundi bora.
Wanamuziki wa Bendi ya Sauti Sol kutoka nchini Kenya likiwasha moto kwenye tamasha la ZIFF 2014 usiku wa kuamkia leo visiwani Zanzibar. Pichani ni Bien Baraza (vocalist) na Willis Austin Chimano (vocalist) wakifanya yao jukwaani. (Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).
Bien Baraza (kushoto) na Willis Austin Chimano (kulia) wakitoa burudani kwenye jukwaa la ZIFF 2014.
Polycarp Otieno (Quitar & Vocalist) akifanya yake ndani ya ZIFF 2014.Sauti Sol watikisa tamasha la ZIFF 2014
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Hivi mbona baadhi ya wasanii wakati mwingine hawavai nguo za kuwasitiri mwili vizuri? mmeshajiuliza?
ReplyDeletemm nshajiuliza sana.kwanini wanaume utakuta wanavaa suti ama nguo nyengine za kusitiri miili yao vyema,ukija kwa kina dada wameziba chuchu na sehemu ndogo ya kiuno then wanasema wanadhalilishwa.mdau wa hapo juu hii ni kazi ya shetani.nshakujibu swali lako.
ReplyDelete