Familia ya Prof. Cuthbert Z. M. Kimambo wa Chuo Kikuu cha Dar e Salaam inatoa shukurani za dhati kwa wale wote walioshirikiana nasi kwa kwa maombi, kwa hali na mali, na kutufariji kwa njia moja au nyingine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mtoto wetu Mpendwa Samwel Cuthbert Kimambo kwa ajali ya gari iliyotokea tarehe 1 Juni 2014.
Shukurani ziwaendee Uongozi na wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Uongozi na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanafunzi wa Chuo cha Kampasi cha Uhandisi na Teknolojia - UDSM, Uongozi na wafanyakazi wa Small Entrepreneurs Loan Facility (SELF) Project, Uongozi na washarika wa Kanisa la CCT Chuo Kikuu Dar es Salaam na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Arusha Mjini, Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Kuu ya Jeshi Lugalo, Jeshi la Polisi Idara ya Usalama Barabarani, Ndugu, Jamaa, marafiki na majirani wote wa Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, na kwingineko ndani na nje ya nchi.
Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyoijua Mwana wa Adamu yuaja.” Mathayo Mtakatifu Sura 24, Mstari wa 44.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...