Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius Likwelile (wa pili kushoto)
akipokea hundi yyenye thamani y ash. Bilioni moja ktoka TIPER gawio la hisa
katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma. Wa kwanza kshoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa TIPER Daniel Belair, Wa pili kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa
Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma na Wizara ya fedha
Kaimu Msajili wa Hazina Elius Mwakabinga (wa kwanza kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER Daniel Belair (kushoto) akitoa taarifa ya
kampuni ya TIPER invyoshikiana na Serikali katika kukuza uchumi na kuongeza
soko la ajira nchini wakati wa kukabidhi gawio linalotolewa na kampuni yake
kwa serikali leo mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma.
Serikali imepokea shilingi bilioni 1.275 kutoka TIPER ikiwa ni gawio ambalo
kampuni hiyo imekuwa ikilipa kwa Wanahisa wake kila mwaka.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servarcius
Likwelile alipokuwa akipokea gawio hilo katika hafla iliyofanyika leo mjini
Dodoma.
Dkt. Likwelile alisema kuwa gawio hilo litaelekezwa kwenye bajeti ya
mwaka huu wa fedha 2013/2014 unaomalizika kwa kuangalia maeneo
ambayo yanawagusa wananchi ikiwemo sekta ya elimu, afya na maji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Daniel Belair
alisema kuwa si mara ya kwanza kwa kampuni yake kutoa gawio kama
hilo kwa Serikali ambapo mwaka jana muda kama huu kampuni ilitoa kiasi
kama hicho kama gawio.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa kampuni yake imeendelea kufanya
vizuri katika kukuza maisha ya kijamii na kiuchumi ambapo kwa sasa
inafanyakazi kwa saa 24 na siku saba za wiki.
Kwa kuzingatia utendaji huo, kampuni ya TIPER imekuwa kichocheo kukuu
cha kuzalisha ajira nchini ambapo hadi sasa asilimia 99 ya wafanyakazi
wake ni nguvu kazi ya Watanzania.
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER Prof.
Abdulkarim Mruma alisema kuwa imekuwa ni muhimu kwa kampuni
yao kuwa na akiba ya kutosha ya mafuta kwa nchi na kuleta mafanikio
makubwa ya upatikanaji wa mafuta nchini.
Aidha, TIPER Prof. Mruma alisema kuwa kwa sasa kampuni yao imejikita
katika kuleta mafuta yaliyosafishwa nchini ili kupunguza gharama
zisizokuwa za lazima.
“Kwa sasa tunaleta mafuta yaliyosafishwa badala ya mafuta ghafi ambayo
yanazalisha tope jingi ambalo limekuwa ni hatari katika kutunza mazingira
yetu” alisema Prof. Mruma
Pamoja na ufanisi huo, kumekuwepo na changamoto za kuboresha
mkataba wa utendaji na usimamizi wa hesabu masuala ambayo wanahisa
wote wawili wanaendelea kuyafanyia kazi kwa madhumuni ya kuwa na
matokeo mazuri zaidi kwa pande zote.
Kiutendaji kampuni ya TIPER inaendeshwa kwa ubia kati ya Serikali ya
Tanzania ambayo inahisa zenye asilimia 50 na Kampuni ya Oryx Energies
SA asilimia 50.
Pamoja na Tanzania Kampuni ya Oryx Energies SA inafanyakazi katika
mnchi mbalimbali duniani ambazo ni Benin, Burkina Faso, Côte d'Ivoire,
Guinea Conakry, Kenya, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Afrika
Kusini, Uhispania (Visiwa vya Canary), Togo, Uganda na Zambia.
Hiyo tarakimu yako uliyoandika hapo haiendani na maelezo uliyotoa.Hiyo SIO bilioni moja.Ongeza umakini katika uandishi wako kuepuka upotoshaji
ReplyDelete