Mwanamuziki maarufu wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania,anatarajiwa kupanda jukwaani katika maonyesho makubwa ya kimataifa ya 5th.International African festival Tubingen 2014,nchi ujerumani. Mwanamuziki huyo nguli wa reggae amepewa nafasi ya pekee ya kutumbuiza mara mbili kwa siku tofauti katika viwanja vya onyesho hilo Festplatz,Europa str. mjini Tubinge kusini mwa ujerumani, ambako maonyesho yatafunguliwa 17.julai 2014 hadi 20.Julai 2014,maonyesho ya Tubingen yategemewa kukusanya umati wa watu zaidi ya 100,000 na yanazishirikisha bendi na wasanii mbali mbali wa nchi za kiafrika.Pia Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbali mbali za kiafrika wameshaanzakuwasili katika mji huo wa Tubingen ,kuudhuria maonyesho hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2014

    Ivi naweza pata sababu kwanini huyu mtu kutopewa heshima staili huko nyumbani???Hii ni levo kubwa yaani nilipokua nasikiliza huu wimbo sikuona tofauti sana na kundi kama culture.....tuna matatizo makubwa sana.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...