Muziki wa dansi wa Tanzania umezidi kufungua ukurusa mpya katka tufe la dunia,
baada ya wasanii na wanamuziki wa Tanzania kutumbuiza katika onyesho la
TFF Rudolstadt 2014,yaliofanyika kuanzia tarehe 3 adi 6 Julai 2014 mjini Rudolstadt,Ujerumani,ambako vikundi mbali mbali vya sanaa na bendi za muziki kutoka Tanzania zilishiriki,zikiwemo bendi ya Black Warriors ikiwashirikisha jukwaani na wakongwe wa muziki akina Mafumu Bilal,Hassan Bichuka,Cosmas Chidumule na wengine,pia Mchiriku ulikuwapo,bila kukosa Kikundi cha ngoma ya Kaya Baikoko kutoka mkoani Tanga, kikundi cha Qwasida "
Tarbiyya Islamiyya" kutoka Zanzibar, Kikundi cha kinamama cha Ngoma za Wagogo kutoka Dodoma, Mambo moto moto band na Segere lao walikuwapo hayo yote yalikuwa mjini Rudolstad, nchini Ujerumani nchi ambayo ndipo makao makuu ya "FFU-Ughaibuni"
Kikundi cha ngoma za asili kutoka Tanzania kikiendelea kutoa burudani katika Tamasha hilo la TFF Rudolstadt 2014,nchini Ujerumani.
Wazee wa Ngoma Baokoko.
Mafumu Bilal Mubenga akifanya yake jukwaani.
Hassan Bichuka na Cosmas Chidumule wakiongoza jukwaa katika Tamasha la TFF Rudolstadt 2014,nchini Ujerumani.
Nyomi la nguvu.
Safi sana Tanzania.
ReplyDeleteUncle hao jamaa tutawapata vipi, waje na huku Nürnberg(Germany) kutumbuiza Tansania Festival tarehe 02 August 2014. Wawasiliane na mimi kwa Email ifuatayo: mulawao@yahoo.co.uk
Mdau,
Erick- Nürnberg.